Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Andy Murray Aondolewa Kwenye Mashindano ya Qatar Open

Murray Andy Andy Murray

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mcheza tennis namba 87 kwa ubora duniani Andy Murray ameondolewa kwenye mashindano ya Qatar ExxonMobil Open baada ya kupoteza kwa mfululizo wa set kwenye hatua ya 16 bora.

Andy Murray alipoteza 6-0, 6-1 dhidi ya Roberto Bautista, kwenye hatua ya robo fainali ya mashindano ya Qatar ExxonMobil Open Bautista anatarajia kukutana kati ya Briton Dan Evans au Alejandro Davidovich Fokina.

Andy Murray alifanikiwa kutinga hatua ya 16 bora kwa kumshinda mchezaji namba 110 duniani Taro Daniel, kwenye ushindi wa set mfululizo wa 6-2, 6-2, mchezaji huyo kutokea nchini Uingereza kwa sasa anafungusha virago vyake na kwenda kujipanga upya.

Andy Murray alianza kuwa mchezaji wa kujitemea mwaka 2005 na amefaanikiwa kuchukua mataji 46 kwa ujumla, huku msimu wake bora ambao alifanikiwa kuwa mchezaji namba moja wa Duniani ni mwaka 2016.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live