Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Andy Murray Anahitaji Kocha Kurejea Kwenye Ubora

Andy Murray Plays A Shot Mcheza tenisi wa Scotland, Andy Murray

Sat, 12 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mcheza Tenisi, Andy Murray bado anaamini ataendeleza ubora katika michezo yake anapojitayarisha kuelekea Doha katika michuano yake ijayo akiwa na kocha Colin Fleming kando yake.

Murray alitengana na mkufunzi wake wa muda mrefu Jamie Delgado kabla ya msimu wa 2022 kabla ya kumaliza kipindi chake cha majaribio na Jan de Witt kufuatia kuondolewa Australian Open na Taro Daniels kutoka Japan.

Bingwa huyo mara mbili wa Wimbledon alikuwa akifanya kazi pamoja na kocha wa zamani Dani Vallverdu huko Rotterdam ambapo Murray alitolewa na kijana chipukizi wa Canada, Felix Auger-Aliassime siku ya Alhamisi.

Raia huyo wa Venezuela, ambaye kwa sasa anamfundisha Stan Wawrinka, ataungana na Murray tena Dubai, lakini ni suluhisho la muda mfupi tu kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34.

“Ninajaribu kupata suluhisho la kudumu ili niwe na ubora katika suala la mambo ambayo ninafanyia kazi kwa sababu kuwa na jumbe tofauti kutoka kwa watu wanaofanya kazi nawe kila wiki sio sawa,” alisema Murray.

Andy amerejea tena ndani ya 100 bora baada ya kukosekana kwa miaka minne, anaamini yuko kwenye njia sahihi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live