Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Adhabu kali zinakuja kwenye tennis -ATP

Nick Kyrgios Racket Nyota Nick Kyrgios

Tue, 5 Apr 2022 Chanzo: eatv.tv

Chama cha wachezaji wa kulipwa kwa upande wa mchezo wa tennis ATP kimesema kitaangazia upya sheria na taratibu za adhabu kwa vitendo vya visivyokuwa vya kimichezo ambavyo hufanywa na wachezaji wakiwa uwanjani na kuweka adhabu kali zaidi ili kulinda hadhi ya mchezo huo duniani.

Mwenyekiti wa ATP Andrea Gaudenzi amewaambia wachezaji wameanza kuangalia tena sheria za kudhibiti vitendo vibaya vya wachezaji pindi wakiwepo uwanjani ikiwemo kuvunja raketi ya kuchezea sambamba na kutoa lugha isiyofaa kwa wasimamizi wa mchezo husika

“kwa miezi mitatu ya msimu huu tumeona vitendo visivyokubalika kwenye michezo ikiwahusisha wachezaji wenye majina makubwa ,vitendo hivi vinatoa athari kubwa  kwa watu wote na vinatoa ujumbe mbaya kwa mashabiki hususani mashabiki wadogo ndio maana tumekuwa na adhabu za haraka na kuelekeza maamuzi kufanyika kwa haraka zaidi kwa kufuata kanuni na taratibu tulizojiwekea “amesema Gaudenzi

Haya yanakuja ikiwa miezi michache imepita tangu nyota wa Australia Nick Kyrgios kupigwa faini ya dollar $60,000 (Tsh million 139,320,000 za kitanzania) baada ya kubamiza raketi yake ya kucheza kwenye michuano ya Indian Wells na Miami Open kwa mwaka 2022 huku Mjerumani Alexander Zverev akiondoshwa kwenye michuano ya Mexico kwa kosa hilo la kubamiza raketi yake ya kuchezea.

Chanzo: eatv.tv