Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Hatujamsamehe Kagoma

Kagoma WA0000 Yanga: Hatujamsamehe Kagoma

Fri, 6 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga Sc, Ally Kamwe amesema taarifa zinaenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa klabu ya Yanga imesamehe mchezaji Yusuph Kagoma ni za uongo na kuwa Shauri kati ya klabu na mchezaji huyo lipo katika Kamati ya Sheria na Hadhi ya wachezaji ya Shiriki la Mpira wa Miguu (TFF).

“Hii taarifa ni ya uongo na hatujui aliyetengeneza alikuwa na dhamira gani hakuna taarifa kutoka Yanga kwamba tumemsaheme mchezaji yeyote wala makubaliano yoyote.

“Ni kweli lipo shauri Kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi ya wachezaji la klabu ya Yanga likimuhusu mchezaji Yusuph Kagoma na taarifa ni kwamba Kamati imekutana na kufanya maamuzi ya kumsimamisha mchezaji asiendelee kutumia Kwenye mechi za timu yake anayoitumikia.

“Kamati yenyewe inashangaa kuona mchezaji bado anatumika huku ana shauri lake chini ya kamati hiyo, nafikiri wadau na wachambuzi wa mpira wa miguu watakuwa na nafasi nzuri ya kutuelezea na kutuchambulia jambo hili,” amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live