Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vieira: AFCON Inastahili Heshima Zaidi

Skysports Vieira Patrick 5545359 Vieira: AFCON Inastahili Heshima Zaidi

Sat, 25 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa klabu ya Crystal Palace, Patrick Vieira amesema kuwa michuano ya AFCON inastahili heshima zaidi.

Vieira anategemea kupoteza wachezaji wake watatu michuano hiyo itakapoanza mnamo Januari 9.

Wachezaji hao ni Cheikhou Kouyate (Senegal) Wilfried Zaha (Ivory Coast) na Jordan Ayew (Ghana).

"Ninaheshimu na kuelewa umuhimu wa wachezaji kwenda kuziwakilisha nchi zao. Hivyo kamwe siwezi kumzuia mchezaji kwenda kwenye AFCON. Ninaamini AFCON inatakiwa kuheshimiwa, maana ina umuhimu sawa na ule wa UEFA," amesema Vieira.

Aidha, Vieira amewataka waandishi wa habari kutoka ulaya kufuatilia AFCON kwa karibu zaidi na kuripoti matukio muhimu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: