Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tiketi zinakimbia fasta fainali Mapinduzi

Fainali Mapinduzi Tiketi zinakimbia fasta fainali Mapinduzi

Sat, 13 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wa soka hapa Unguja hawataki kusimuliwa, wameamua kuja wenyewe kutazama fainali ya Kombe la Mapinduzi wakimiminika kwa wingi kuja kununua tiketi za mchezo huo.

Hapa Uwanja wa New Amaan Complex kuna mistari mirefu ya mashabiki wanaokwenda kununua tiketi za mchezo huo wa fainali kati ya bingwa mtetezi Mlandege ya hapa Zanzibar dhidi ya Simba utakaopigwa kuanzia saa 2:15 usiku.

Mashabiki hao wamegawanyika ambapo wengi wapo wa Simba na wengine wa Mlandege wakiwemo pia wa klabu zingine wanaotaka kuwa sehemu ya fainali hiyo ya kwanza kwenye uwanja huo uliofanyiwa maboresho makubwa.

Iko hivi, muamko mkubwa wa mashabiki hao unatokana na kupanuliwa kwa uwanja huo ambao sasa unaingiza mashabiki wengi zaidi kuliko miaka iliyopita.

Uwanja wa Amaan hapo awali ulikuwa unachukua takribani mashabiki 12,000 na baada ya maboresho hayo makubwa unachukua watazamaji 15,200.

Tambo za mashabiki wa timu pinzani zimekuwa zikiendelea kwa kila timu kutamba kwamba itamfunga mwenzake kwenye fainali hiyo.

Simba imekuwa ikipita mitaa mbalimbali kuanzia asubuhi ikiwahamasisha mashabiki wake kwenda kuujaza uwanja wakisaka taji la pili msimu huu baada ya awali kuchukua Ngao ya Jamii mbele ya watani wao Yanga kwa matuta pale Uwanja wa CCM Mkwakwani mkoani Tanga.

Chanzo: Mwanaspoti