Tue, 20 Jun 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Uongozi wa Klabu ya Simba SC umetangaza kuachana na mlinzi wa Kati Mohammed Outtara raia wa Ivory Coast.
Outtara alisajiliwa na Simba SC Julai 2022 kutoka Al Hilal ya Sudan kwa Mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka mwingine.
Kuondoka kwa Outtara nis sehemu ya marekebisho ya kikosi cha Simba SC yanayofanywa kuelekea msimu ujao 2023/24.
Outtara anakuwa mchezaji wa tatu kuachwa na Simba baada ya Augustine Okrah na Victor Akpan.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: