Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TP Mazembe yaiomba Yanga iwaazimishe mshambuliaji huyu

Katumbi Sdc TP Mazembe yaiomba Yanga iwaazimishe mshambuliaji huyu

Fri, 6 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa TP Mazembe, Moise Katumbi ameiomba klabu ya Yanga kupitia kwa Rais wa Yanga Eng. Hersi Saidi wawaazime mshambuliaji wao mpya, Sabinah Tom.

Klabu ya Yanga Princess imemsajili mshambuliaji tegemeo wa klabu ya TP Mazembe, Sabinah Tom ambaye ni top scorer wa ligi ya Dr Congo na ameisaidia klabu ya TP Mazembe kufuzu ligi ya mabingwa Africa msimu huu.

Uongozi wa TP Mazembe umeiomba klabu ya Yanga wamtumie Mchezaji huyo kwenye fainali za ligi ya mabingwa Africa hadi klabu hiyo itakapoishia kisha ajiunge na klabu yake mpya ya Yanga Princess.

Rais wa klabu ya Yanga SC, Eng. Hersi Said amekubali ombi hilo. Ameamua kuweka nguvu pia kwenye timu ya Wanawake ya Yanga Princess ambapo hadi sasa wachezaji hawa wakigeni wamesajiliwa.

Sabinah atahudumu TP Mazembe kama mchezaji wa mkopo kutoka Yanga Princess.

Rita Akarekor.

Golikipa timu ya Taifa Nigeria.

Uzoamaka Igwe Confidence

➜ Beki wa kati timu ya Taifa ya Nigeria.

➜ (CAF) Bronze medalist

Toluwashe Adeshola

➜ Kiungo timu ya Taifa Nigeria.

➜ (MVP) ligi kuu ya Nigeria.

Danai Bhobho

➜ Kiungo timu ya Taifa ya Zimbabwe.

Sabinah Tom

➜ Striker timu ya Taifa ya Malawi

➜ Striker klabu ya TP Mazembe.

➜ Top scorer 2023|24.

Usajili unaendelea....

Ligi ya wanawake Tanzania bara itaanza rasmi baada ya nusu fainali za Ngao ya jamii zitakazofanyika kuanzia 24 - 27 September ambapo Simba Queens na Yanga Princess watakutana kwenye mechi hizo za ufunguzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live