Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sub' yaiua Ghana nyumbani, mashabiki warusha chupa

Angola Sas Sub' yaiua Ghana nyumbani, mashabiki warusha chupa

Fri, 6 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukistaajabu ya Taifa Stars utashangaa ya Black Stars ya Ghana baada ya timu hiyo kukubali kipigo cha bao 1-0 nyumbani kutoka kwa Angola.

Kikosi cha Ghana

Ghana licha ya kutawala mchezo wa kuwania fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) 2025, kwa dakika zote 90, lakini ikajikuta ikiruhusu bao pekee dakika ya tatu kati ya tano za nyongeza likifungwa na mtokea benchi, winga wa kushoto, Felicio Milson.

Bao hilo la Angola limetengenezwa na wachezaji wawili walioingia kwa mabadiliko kipindi cha pili, ambapo asisti imetoka kwa winga wa kulia, Zito Luvumbo aliyeingia dakika ya 60 akichukua nafasi ya Randy Nteka.

Vurugu za mashabiki uwanjani

Milson aliingia dakika ya 76 akichukua nafasi ya mshambuliaji Agonstinho Paciencia 'Mabululu' akitumia dakika 17 kwenda kuitengenezea ushindi Angola katika mchezo wa kuwania fainali hizo zitakazofanyika  Morocco.

Baada ya bao hilo mashabiki wa Ghana ambao walijaa katika Uwanja wa Baba Yara jijini Kumasi wakisubiri ushindi wa Black Stars wakajikuta wanachukizwa na matokeo hayo na kuamua kurusha chupa uwanjani.

Ghana vs Angola

Ghana itarudi tena uwanjani ikiwa ugenini Jumatatu kukabiliana na Niger iliyoteleza mbele ya Sudan kwa kufungwa bao 1-0 juzi katika mechi nyingine ya Kundi F.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live