Kajla ya juzi Jumamosi Simba SC haijacheza dhidi ya Horoya AC ya Guinea katika mchezo wa Kundi C kunako Ligi ya Mabingwa Afrika, timu hiyo ilikuwa imefunga mabao mawili pekee baada ya kushuka dimbani mara nne.
Kutokana na ufinyu wa mabao katika michuano hiyo inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, amewakingia kifua mastaa wa kikosi hicho.
Simba katika mabao hayo mawili hatua ya makundi, wafungaji ni beki Henock Inonga na kiungo Clatous Chama, huku washambuliaji, Moses Phiri, Jean Baleke, Kibu Denis, John Bocco na Habib Kyombo wakiwa hawajafunga.
Akizungumzia hilo, Robertinho, alisema: “Katika soka, huwezi kufunga kila nafasi, nimecheza mpira na ninaufundisha kwa sasa, ninahitaji itokee hivyo, lakini inashindikana.
“Kikubwa ambacho ninashukuru kuona ndani ya Simba tunacheza mpira mzuri katika michuano ya ndani ya kimataifa, sio rahisi kushinda ugenini na nyumbani dhidi ya Vipers.
“Hayo mambo mengine yanakuja taratibu na naamini kutokana na vipaji walivyonavyo wachezaji wangu, hali itakaa vizuri siku si nyingi.”