Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Molina: Madrid wanajuta kumsajili Mbappe

Molina Molina: Madrid wanajuta kumsajili Mbappe

Mon, 21 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwandishi wa habari wa Uhispania Romain Molina amedai kuwa Real Madrid 'inajuta' kumsajili Kylian Mbappe kutoka PSG huku wakionyesha kushangazwa na kiwango chake cha uchezaji kwasasa.

Inasemekana pia kwamba kocha wa Madrid Carlo Ancelotti na wajumbe wa bodi walipinga sana kusainiwa kwa Mbappe lakini Rais wa klabu hiyo Florentino Perez ndiye aliyeng'anganiza.

Akiongea na Cointerview, Molina amesema

"Wanajuta kumleta. Haijawa kama walivyotarajia. Alikuwa ni kipenzi cha Florentino Perez. Ni Perez pekee ambaye amekuwa akiwapenda wachezaji wakubwa.. Nadhani Real wamefanya makosa makubwa sana" anamalizia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live