Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Minziro apewa mikoba ya Kapunovic Pamba Jiji

Image 377 1140x640 Minziro Felix.png Kocha Fred Felix Minziro

Thu, 17 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Pamba Jiji Fc imethibitisha kumteua kocha Fred Felix ‘Minziro’ kuwa Kocha Mkuu akichukua mikoba ya Goran Kopunovic aliyetupiwa virago Oktoba 16, 2024.

Taarifa ya leo Oktoba 17, 2024 iliyotolewa na Kaimu C.E.Ο kwa klabu hiyo, Ezekiel Ntibikeha imebainisha kuwa Minziro atashirikiana na Kocha msaidizi Mathias Wandiba.

“Uongozi wa Pamba Jiji Fc unawatakia kila la kheri katika kipindi hiki cha kazi yao mpya, huku wanamwanza wakiwa na matumaini kibao ya kuiona Pamba Jiji ikifanya vizuri Ligi Kuu.” — imesema taarifa hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live