Serikali imesema kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023 Mfuko wa Utamaduni na Sanaa ulipokea maombi ya mikopo yenye thamani ya Tsh. 9,262,096,578 (Bilioni 9.2) kutoka kwa waombaji 219.
Hadi Aprili 2023 mikopo iliyotolewa ni ya Tsh. 1,077,000,000 kwa miradi 45 kutoka maeneo mbalimbali ya Sekta ya Utamaduni na Sanaa. 33.
Akiwasilisha Bungeni makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Mwaka 2023/24 ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt. Pindi Chana amesema jumla ya ajira 21,579 zikiwemo 733 za kudumu na ajira za muda ni 20,846
Aidha, Mfuko umekuwa kichocheo kikubwa kwa wadau katika eneo la urasimishaji kwani umewahamasisha kurasimisha shughuli zao katika mamlaka mbalimbali kama vile Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Halmashauri pamoja na mamlaka nyingine za udhibiti ili waweze kuendesha shughuli zao kibiashara.