Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgunda akabidhiwa shoo ya Yanga

Mgunda Simba Gd Mgunda akabidhiwa shoo ya Yanga

Tue, 4 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabosi wa Simba wameshtukia jambo zito baada tu ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufanya mabadiliko ya haraka kwa kuamua kumkabidhi timu kocha msaidizi ya timu hiyo, Juma Mgunda kuelekea katika mchezo dhidi ya Yanga inayoonolewa Nasreddine Nabi raia wa Tunisia.

Simba imefanya mabadiliko hayo ya ndani baada ya kumaliza mchezo wao dhidi ya Raja Casablanca kwa kumpa madaraka Mgunda kwa lengo la kuongoza maandalizi ya mchezo ambao kwa msimu wa tatu sasa Simba hajawahi kuambulia ushindi mbele ya Yanga.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya viongozi wa juu wa Simba zinadai kuwa tayari wameshamkabidhi timu kocha huyo kwa kuwa ana uwezo mkubwa wa kucheza mechi yao na watani wa jadi kufuatia uzoefu wake katika Ligi Kuu Bara.

Mtoa taarifa alienda mbali kwa kusema kuwa kwa sasa kocha Roberto Oliveira 'Robertinho' atakuwa akifanya kazi ya kushauri na kuongoza mambo mengine lakini sehemu kubwa ya maandalizi ya mchezo huo itakuwa chini ya Mgunda ambapo ataanza katika mchezo wao ujao katika Kombe la FA dhidi ya Ihefu.

"Maandalizi ya kuelekea katika mchezo wetu na Yanga tayari yameanza baada ya mechi yetu na Raja kumalizika kwa sababu viongozi wa juu walikaa kikao na kuona inafaa hii mechi, kocha Mgunda ndiyo aongoze jahazi katika mipango yote.

"Unajua mabosi wameangalia mambo mengi ya kimsingi na kiufundi lakini suala la uzoefu wa kujua asili mechi ya watani ilivyo tofauti na kocha mkuu ambaye bado mgeni na kazi itaanza katika mechi mbili za Ihefu ile ya Ligi na ina FA kabla ya kucheza na Yanga katika mchezo ambao viongozi wanataka wakiona matokeo mazuri yanapatikana,” alisema mtoa taarifa.

Lakini alipoulizwa, Robertinho juu ya suala hilo alisema: "Ninachokiangalia kwa sasa ni kuweza kushinda hatua ya robo fainali ya Kombe la FA kisha kushinda mchezo wetu wa ligi na Ihefu kisha hao Yanga kwa sababu hizi mechi zote hakuna nyepesi kwetu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: