Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchezaji asafiri kwa ndege kwa dakika 8 kwenda mazoezini kila siku

Dnjuma Dd Mchezaji asafiri kwa ndege kwa dakika 8 kwenda mazoezini kila siku

Sat, 13 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Everton, Sean Dyche amelazimika kukaa kitako na mchezaji Arnaut Danjuma kutokana na uamuzi wa staa huyo kusafiri kwa ndege kutoka jiji la Manchester hadi Liverpool umbali wa dakika nane tu kwenda mazoezini.

Mchezaji huyo aliyetoka Villarreal kwa mkopo Danjuma aliripotiwa kusafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Manchester hadi wa Liverpool kwenda kukutana na wachezaji wenzake kwa ajili ya mazoezi.

Na umbali wa safari hiyo ni dakika nane tu, hivyo Danjuma amekuwa akipanda ndege kwenye safari ya dakika nane. kitu ambacho kimeshangaza wengi, huku wengine wakisema "siku hizi hakuna wanamichezo."

Dyche alisema alilazimika kukaa kitako na winga huyo kutokana na safari zake zake.

Kocha, Dyche, 52 alizungumzia walivyo wachezaji wa kisasa na kusema: "Nilizungumza naye. Nilimwambia ni kujipandisha sana kusafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Manchester hadi uwanja wa ndege wa Liverpool kuja mazoezini. Kama unavyojua, hawa ni wachezaji wa kizazi hiki...Binafsi ningetumia gari, lakini hao ni wachezaji wetu wa siku hizi. Unajua, wanataka kujilinda zaidi na kupenda mapumziko."

Mashabiki walishtuka sana baada ya kusikia Danjuma amekuwa akisafiri kwa ndege kwenye safari ya dakika nane, ambapo shabiki wa kwanza aliandika kwenye Twitter: "Mchezaji wa kiwango D anasafiri kwa ndege kwenda mazoezini kila siku…michezo imekwisha."

Mwingine alisema: "Bwanaee." Shabiki wa tatu alishangaa, akiliuza: "Kweli?"

Kuna shabiki mwingine alisema: "Huyo mtu ni nani?"

Na mwingine aliongeza: "Hiyo ni mbaya, yani safari ya kuendeesha gari hata saa halifiki."

Danjuma alijiunga na Everton kwa mkopo baada ya kushindwa kung'ara kwenye kikosi cha Tottenham Hotspur msimu uliopita ambapo alipelekwa pia na Villarreal.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, amekuwa akizivutia timu nyingi ikiwamo Lyon, ambayo inataka kumsajili kwenye dirisha hili la Januari. Hata hivyo, Everton hawapo tayari kumwaacha mchezaji huyo hasa baada ya Dwight McNeil kuwa majeruhi.

Chanzo: Mwanaspoti