Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe ashtushwa na tuhuma za ubakaji

Mbappe Kylian Rape Mbappe ashtushwa na tuhuma za ubakaji

Thu, 17 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa timu ya Taifa ya Ufaransa Kyllian Mbappe ameeleza kushtushwa kwake na taarifa zinazomhusisha na ubakaji uliotokea nchini Sweden.

Mamlaka nchini Sweden zimethibitisha kuwa upo uchunguzi unaoendelea kuhusu tukio la ubakaji lilitokea kwenye hoteli iitwayo Bank , Oktoba 10.

Vyombo vya habari nchini humo vimemtaja Mbappe kuwa ndiye anayehusishwa na tukio hilo na alikuwepo jijini Stockholm wiki iliyopita katika hoteli ambayo polisi wameitembelea kama sehemu ya uchunguzi.

Shirika la habari la SVT la nchini Sweden limeeleza kuwa vipo viashiria vya kuridhisha kuwa tukio hilo lililotokea, hata hivyo mshukiwa hajatajwa.

Mwanasheria wa Mbappe amelaani vikali tetesi hizo na kueleza kuwa zina nia ya kumchafua mwanasoka huyo.

Aidha, Mwanasheria huyo amesema Mbappe yupo katika hali ya utulivu kwani anajua hahusiki na suala hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live