Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuhusu rekodi ya kadi, Maresca asema jambo

Marescaaaaa Kocha Mkuu wa Chelsea, Enzo Maresca

Mon, 16 Sep 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AFC Bournemouth kocha wa Chelsea, Enzo Maresca amefunguka kuhusu rekodi ya kadi iliyowekwa kwenye mechi hiyo.

Chelsea ambayo ilifanikiwa kupata ushindi kupitia bao lililofungwa na Christopher Nkunku dakika za lala salama ilifikisha pointi saba na kupanda hadi nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Lakini mchezo wa Jumamosi pia ulitengeneza rekodi ya kadi nyingi za njano katika historia ya Ligi Kuu England.

Hapo awali mechi iliyokuwa imezalisha kadi nyingi zaidi za njano ilikuwa ni kati ya Wolves vs Newcastle mwaka 2010 kulipokuwa na kadi 12 sawa na pambano la mwaka 2016 kati ya Chelsea na Tottenham katika pambano mechi iliyopewa jina la Battle of the Bridge, pia mchezo wa msimu uliopita kati ya Tottenham na Sheffield United.

Rekodi hizo zote zilivunjwa na mechi hiyo ya Chelsea na Bournemouth ambapo kulikuwa na kadi za njano 14 zikitolewa na mwamuzi anayesifika kwa kadi Anthony Taylor ingawa hakukuwa na mchezaji au kocha aliyetolewa nje kwa kadi nyekundu.

Kijumla Tayler alionyesha kadi za njano mara 16 lakini mbili ziliuwa ni kwa makocha wa timu zote na zilizobaki zikaenda kwa wachezaji.

Kocha wa Chelsea alisema:"Nililalamika kuhusu kuchezewa vibaya kwa Wesley Fofana jambo ambalo kwangu lilikuwa wazi,"alisema Maresca ambaye alisisitiza kwamba kutolewa kwa kadi nyingi za njano yeye aliona ni kawaida.

Baada ya mechi kocha wa Bournemouth Andoni Iraola alikataa kuzungumza kuhusu mwamuzi wa mechi hiyo.

"Nimekuwa nikizungumza na haifanyi kazi kwa hivyo nimeamua sasa nitajaribu kinyume chake(nisizungumze), nione nini kitatokea,"alisema Iraola.

Chanzo: Mwanaspoti