Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni za betting wadhamini vilabu ili kupewa leseni

TARIMBA WEB Kampuni za betting wadhamini vilabu ili kupewa leseni

Tue, 6 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge Jimbo la Kinondoni, Abbas Tarimba amesema kuwa Serikali iweke utaratibu ambao utazilazimu kampuni za michezo ya kubashiri kudhamini timu za Ligi Kuu au Championship ili kupewa leseni.

Tarimba ambaye pia ni kiongozi mwandamizi wa Klabu ya Yanga na Mkurugenzi wa Kampuni ya betting ya SportPesa amesema hayo leo bungeni Dodoma wakati akichangia hoja kuhusu bajeti ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

"Sports Betting inategemea sana mpira wa miguu, hapa Tanzania, 90% ya wanaocheza Betting, wanabet katika mpira wa miguu, hivyo industry ile inafaidika na mpira wa miguu, tunarudisha nini?

"Kwa hali hii nilikuwa nashauri serikali, iwe ni sharti la kikanuni kupata leseni kwa makampuni ya betting, ilazimike kudhamini Premier Club ama Championiship Club, hapo tutakwenda kusaidia nchi yetu katika michezo," amesema Abbas Tarimba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: