Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi ampa tano Chama Ligi ya Mabingwa Afrika

Chama 52 Gamondi ampa tano Chama Ligi ya Mabingwa Afrika

Mon, 26 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amempa tano Clatous Chama pamoja na wachezaji wengine kwa kucheza katika kiwango bora mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vital’O.

Yanga inatinga Hatua ya Pili Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa jumla ya mabao 10-0 Vital’O kwa kuwa kwenye mchezo wa kwanza wakiwa ugenini ilikuwa Vital’O 0-4 Yanga na ule wa pili wakiwa nyumbani ilikuwa Yanga 6-0 Vital’O.

Chama ambaye aliibuka Yanga akitokea Simba ni mabao sita kahusika akifunga mawili na kutoa jumla ya pasi nne za mabao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika katika mechi mbili ambazo ni dakika 180.

Gamondi amesema kuwa wachezaji wanajituma uwanjani katika kutimiza majukumu yao jambo ambalo wanastahili pongezi na mchezo dhidi ya Vital’O ule wa pili walicheza katika kiwango bora.

“Pongezi kwa wachezaji wanajituma na kufanya kazi kubwa uwanjani kwenye mchezo wetu tukiwa nyumbani dhidi ya Vital’O walicheza kwenye kiwango bora ambacho kinafurahisha na kinapaswa kuwa endelevu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: