Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Tumefika salama Kagera, tuko tayari kwa kazi

Gamondi Chama Boka Gamondi: Tumefika salama Kagera, tuko tayari kwa kazi

Wed, 28 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa timu ya Yanga SC, Miguel Gamondi amesema watapambana kuhakikisha wanashinda mechi yao kesho dhidi ya Kagera Sugar.

Gamondi amesema Kagera Sugar ni moja ya timu imara katika ligi, lakini wako tayari kwa ajili ya kupambana nao.

“Tumefika salama na tumejiandaa vya kutosha, tunakwenda kuanza msimu mpya tukiwa na hamasa kubwa. Sitaki kuangalia sana mchezo uliopita ingawa tulipata somo. Tumeshajiandaa kisaikolojia kucheza dhidi yao kwa kuzingatia namna yao ya uchezaji na mazingira ya uwanja.

“Huu ni mwanzo wa msimu, nimeshawaeleza wachezaji wangu nini mashabiki wanahitaji. Kiufupi wananchi wanahitaji alama tatu. Nafahamu mashabiki wetu wanatamani kweli tufunge magoli mengi, lakini kwetu sisi jambo la kwanza ni alama tatu,” amesema Miguel Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: