Kukumbushana si jambo baya kwamba si mara ya kwanza mchezaji kutoka katika kikosi cha Simba kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa kutoka Magharibi mwa Afrika.
Unamkumbuka William Fanbullah (pichani wa pili kulia), aliitwa Liberia kipindi kile cha George Weah (katikati ambaye kwa sasa ni Rais wa Taifa hilo) akiwa on fire Arsenal. Sisemi suala la Sakho kuitwa Lions of Teranga ionekane ni jambo la kawaida sana.
Bado kuna jambo la kuliangalia kwamba scout ya Simba ambayo tumesema Imekuwa ikikosea kuna sehemu imefanya jambo kubwa.
Angalia Senegal, Mabingwa wa Afrika lakini wenye timu mabingwa wa Afrika kwa vijana bado wanaweza kutoa nafasi kwa Sakho wa Simba. Ukubali kwanza Simba inafuatiliwa kwa kuwa lazima wamfuatilie Sakho kabla ya kumteua.
Binafsi niliwahi kufikiri iwapo Sakho atapata nafasi ya timu ya taifa inaweza kuinua zaidi mwendo bora wa kiwango chake.
Anyway, Simba inakwenda kutengeneza rekodi ya kuwa na mchezaji kwenye kikosi cha mabingwa wa Afrika ni jambo zuri na linaitangaza klabu.
Pia, kwa wengine walio Simba, ninaamini hiyo ni sindano ya kuamini wakicheza kwa ubora nafasi itapatikana.