Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi: GSM aombewe badala ya kupigwa vita

Herwi GSM 098793145 Eng. Hersi: GSM aombewe badala ya kupigwa vita

Tue, 27 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa kama kuna mtu ambaye mashabiki wanapaswa kumpongeza na kumuombea ni mfadhili wa Klabu hiyo, Ghalib Said Mohammed ‘GSM’ kwani amekuwa msaada mkubwa kwa mafanikio ya klabu ambayo imekuwa ikiyapata tangu aanze kuwapa fedha.

Hersi amesema kuwa badala ya kuwaponda wadhamini hao kwa kudhamini vilabu mbalimbali, wanapaswa kuwatia moyo na kuendelea kuwapokea kwani vilabu vyote vya soka nchini vinahitaji wadhamini, wawekezaji na mafadhili ili kujiendesha na kupata mafanikio, vinginrvyo hakuna klabu hata moja kwa Tanzania ambayo inaweza kusimama na kujiendesha kwa pesa zake yenyewe.

“Tumekuwa na mahusiano mazuri ya wadhamini wetu ambao kila tunapowakimbilia wanatushika mkono, nichukue fursa hii kuwashukuru sana Kampuni ya SportPesa, Azam TV na GSM kwa kuwa na sisi katika kipindi chote cha Uongozi wangu.

“Kama kuna jambo ambalo Wanayanga wanapaswa kuliombea dua liendelee ni uwepo wa GSM kwenye timu yetu, amekuwa akitusapoti katika mambo mengi mno.

“Mfano juzi kwenye Ngao ya Jamii kabla ya kuwashughulikia watu fulani, alikuja na kutuuliza bajeti ya Bonasi ikoje, tulipomwambia akasema haitoshi, akaongeza fungu la maana vijana wakaenda kupambana tukashinda,” amesema Eng Hersi Said.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: