Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cristiano Ronaldo, Lionel Messi namba hazidanganyi

Ronaldo Na Messi Vxv Cristiano Ronaldo, Lionel Messi namba hazidanganyi

Mon, 16 Sep 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Acha maneno weka data. Mjadala wa nani zaidi baina ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, mvutano ni mkubwa. Kwenye maneno, kila mtu atavuta upande wake, lakini mambo yapoje kwenye data. Wanasema namba hazidanganyi.

Namba zinasema hivi, Messi kwenye maisha yake ya soka hadi sasa amecheza mechi 1070, wakati Ronaldo amecheza mechi 1238.

Kwenye mechi hizo, Messi amefunga mabao 840, wakati Ronaldo mabao 901.

Messi ameasisti 375, wakati Ronaldo ameasisti mara 254. Kwenye maisha yao ya soka, Messi amefunga hat-trick 57 na Ronaldo ametupia hat-trick 66. Messi amechaguliwa Mchezaji Bora wa Mechi mara 328, wakati Ronaldo amechaguliwa mara 178, huku kwenye upande ya mabao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ronaldo amefunga 141 na Messi 129.

Kwenye soka la kimataifa, Messi amechaguliwa kuwa bora mara tano, wakati Ronaldo hajawahi kushinda tuzo ya ubora kwenye soka la kimataifa, huku Messi akishinda mataji 45 na Ronaldo mataji 33. Messi ameshinda Ballon d’Or nane, wakati Ronaldo amebeba tuzo hizo mara tano. Messi ameshinda Kiatu cha Dhahabu cha Ulaya mara sita, wakati Ronaldo ameibuka kinara wa mabao kwenye ligi za Ulaya mara nne. Kwenye ishu ya kufunga na kuasisti kwenye mechi za fainali, Messi amefanya hivyo mara 50 na Ronaldo mara 25, huku supastaa Messi akifunga mabao 65 kwa mipira ya adhabu na Ronaldo amefunga aina hiyo ya mabao mara 64. Kwenye soka la kimataifa, Messi amefunga mabao 109, wakati Ronaldo ametupia nyavuni mara 132, huku mataji waliyobeba kwenye soka la kimataifa, Messi amefanya hivyo mara nne na Ronaldo mara mbili.

Hizo ni rekodi ya mechi zote, ambapo Messi amecheza kwenye kikosi cha Barcelona, Paris Saint-Germain, Argentina na Inter Miami - huku Ronaldo akicheza kwenye vikosi vya Sporting CP, Manchester United, Real Madrid, Juventus, Al Nassr na Ureno.

Chanzo: Mwanaspoti