Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baleke amuondoa Katwila Ihefu

Baleke Katwila Baleke na Katwila

Thu, 13 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kitendo cha straika wa Simba, Jean Baleke kupeleka kilio mara mbili ndani ya Ihefu, kimetajwa kuwa ni sababu ya mabosi wa klabu hiyo kuachana na Kocha Zubeir Katwila.

Baleke ameifunga Ihefu mabao matano katika mechi mbili walizocheza hivi karibuni.

Alianza katika Kombe la Shirikisho la Azam Sports kwa kufunga mabao matatu wakati Simba ikishinda 5-1, Uwanja wa Azam Complex, Dar, kisha Ligi Kuu Bara, Simba iliposhinda2-0, yeye kafunga yote mawili.

Mechi ikichezwa Highland Estate, Mbeya. Imeelezwa kwamba, Katwila ambaye anasimama kama kocha msaidizi ndani ya Ihefu huku John Simkoko akiwa mkuu, alipishana kauli na bosi mkubwa wa timu hiyo.

Chanzo kutoka kwa mtu wa karibu na kocha huyo, kimeeleza kwamba, kupishana kauli huko kulikuja katika upangaji wa kikosi katika mchezo wa kwanza uliochezwa Aprili 7, mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, Dar.

“Wakati kocha amepanga kikosi, bosi aliuliza utimamu wa kipa Shaban Kado ambaye hakucheza mechi kadhaa nyuma, kocha akasema asiingiliwe majukumu yake.

“Baada ya mechi kumalizika na matokeo kuwa 5-1 huku Kado akiruhusu mabao manne ndani ya dakika 45, bosi alikasirika sana, akamwambia Katwila akae pembeni, asiwepo kwenye maandalizi ya mechi ya ligi.

“Muda mchache, akamtaka aungane na timu kwa sharti la kwamba akipoteza mechi hiyo, basi safari yake imefika mwisho.

“Hapa tulipo tunasikilizia kuona kama bosi ameshikilia uamuzi wake au kama atabadilisha, lakini kauli yake ya kwanza ni kwamba tukipoteza mechi ya nyumbani dhidi ya Simba, basi Katwila hana chake tena.

“Unajua Katwila ni kocha msaidizi, lakini ana majukumu kama kocha mkuu, uwepo wa Kocha Simkoko ni kama kumlinda kwa sababu Katwila bado anasoma, hajafikia vigezo vya kukaa benchi kama kocha mkuu,” alisema mtoa taarifa huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: