Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Mkwe afunguka Ndoa ya binti yake na Sadio Mane

Baba Mkwe Mane Baba Mkwe afunguka Ndoa ya binti yake na Sadio Mane

Sat, 13 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Senegal Sadio Mane aliandaa ndoa yake na mrembo akiwa bado mdogo na hawakufanya chochote hadi hapo walipofunga pingu za maisha hivi karibu, anafichua baba mkwe.

Mane, 31, alifunga ndoa na mrembo Aisha Tamba, 18, katika sherehe za siri zilizofanyika Keur Massar, Jijini Dakar, siku chache kabla ya kuanza kwa fainali za Afcon 2023 huko Ivory Coast.

Wawili hao walikutana kupitia wakala wa Mane, ambaye ni rafiki wa baba yake mrembo Aisha, Amadou Tamba, ambapo kwa kipindi hicho binti huyo alikuwa na umri wa miaka 16.

Tamba alisema alitambulishwa kwa Mane miaka miwili iliyopita na kusema mtoto wake kwa sasa umri wake ni miaka 18. Awali ilidaiwa wawili hao wamekuwa kwenye uhusiano kwa siri, lakini Tamba alisema Mane na Aisha hawajawahi kuwa na uhusiano kabla ya kuoana.

Baba huyo alisema: “Mke wangu na Aisha walitembelea familia ya Mane, na huko ndiko walikokutana kwa mara ya kwanza. Aliona kitu kwa binti yangu na wazazi wake wamemkubali. Walikuja kwangu tuonane. Tulijadili kiasili na tulikubaliana atamsubiri hadi wakati ufike. Hawakuwa na uhusiano kwa sababu Aisha bado mdogo.”

Wawili hao walifikia makubaliano wakati mrembo Aisha akiwa bado shule, lakini familia zao zilikubaliana hadi hapo alifikia umri wa miaka 18, lakini Mane alikuwa akimhudumia mrembo wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live