Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Live Radio

Afrika

Nchi

Kijamii

Aziz Ki: Sasa ni muda wa kwenda kwenye kilele cha Afrika

Aziz Ki Simba Yanga Aziz Ki: Sasa ni muda wa kwenda kwenye kilele cha Afrika

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Stephanie Azizi Ki amemshukuru Rais wa Klabu ya Yanga ambaye pia ni rafiki yake, Eng. Hersi Said kwa kumwamini na kumpa nafasi ndani ya kikosi hicho huku akisema kuwa malengo yao sasa ni kufanya vizuri kimataifa.

Aziz ambaye alisajiliwa na Yanga akitokea ASEC Mimosas mwanzoni mwa msimu uliopita amesema hayo baada ya Yanga kutwaa ubingwa juzi mara ya 30 huku ikiwa ni mara ya pili kwa Aziz Ki kutwaa ubingwa huo akiwa na Yanga.

"Ahsante sana boss, kumbe nilikuwa sahihi kukuamini katika miaka miwili hii ya maajabu. Ahsante kwako sasa tusogee kileleni mwa Afrika, ndio kipaumbele chetu na kila kitu kipo mkononi mwako jamaa yangu," amesema Azizi Stephanie Ki.

Yanga msimu uliopita walicheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika lakini msimu huu wameingia hatua ya makundi na kucheza robo fainali ambapo waliondolewa na Mamelodi Sundowns kwa changamoto ya mikwaju ya penati na malengo yao ni kufanya vizuri zaidi msimu ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live