Sat, 13 Jan 2024
Chanzo: Mwanaspoti
Azam FC ni kama imenogewa na wachezaji kutoka Colombia, kwani kama mambo yatakwenda sawa, muda wowote watamtangaza beki kutoka nchini hiyo.
Hivi karibuni Azam FC ilimtangaza mshambuliaji Franklin Navarro (24) iliyemsajili kutoka Cortuluá FC ya Daraja la Pili ya nchini kwao, Colombia.
Habari kutoka ndani ya kikosi hicho, zinasema viongozi wanatarajia kumsainisha beki, huku jina lake likifichwa sana.
"Wanamalizana na beki raia wa Colombia na wanaweza wakamtangaza muda wowote kuanzia sasa, huyo atakuwa wa pili baada ya kumsainisha mshambuliaji Navarro," kimesema chanzo hicho.
Chanzo: Mwanaspoti