Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal warahisishia kazi ya kumpata Semenyo

Antoine Semenyo 1 Antoine Semenyo

Mon, 21 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Arsenal ni miongoni mwa klabu ambazo zimehusishwa kutaka kumnunua mshambuliaji wa Bournemouth, Antoine Semenyo, ambaye kiwango chake pia kimeripotiwa kuzivutia Tottenham Hotspur na Newcastle United.

Hata hivyo Arsenal huenda wakawa na nafasi nzuri zaidi ya kupata huduma ya Semenyo baada ya mchezaji huyo kunukuliwa akisema yeye ni shabiki mkubwa wa Arsenal kwakuwa ni timu ambayo amekuwa akiifwatilia maisha yake yote.

Alipoulizwa ikiwa kujiunga na Arsenal ni ndoto yake, Semenyo alisema: "Ndio, timu yoyote ile inayocheza Ligi ya Mabingwa au Europa...hilo ndilo lengo langu.

Football Insider imeripoti kwamba Bournemouth wako tayari kupokea dau lisilopungua pauni milioni 40 mpaka 50.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live