Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arne Slot awalaumu mastaa wake

Skysports Liverpool Arne Slot 6685695 Arne Slot awalaumu mastaa wake

Mon, 16 Sep 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Liverpool Arne Slot amesema wachezaji wake wanapaswa kulaumiwa kutokana na kipigo ambacho timu hiyo ilikipokea dhidi ya Nottingham Forest.

Kabla ya kupoteza mechi hiyo, Liverpool ilishinda mechi zao tatu za kwanza za ligi chini ya Slot bila ya kuruhusu bao hata moja.

Majogoo hawa walipiga mashuti 14 dhidi ya matano ya wapinzani wao lakini hawakuweza kufanikiwa kutikisa nyavu za Matz Sels.

Baada ya kipigo hicho Liverpool ilisalia nafasi ya pili kwenye msimamo kwa pointi zao tisa ikiwa ni tofauti ya alama tatu dhidi ya vinara Manchester City.

"Matokeo haya yanakatisha tamaa zaidi na hatuwezi kufurahia jinsi mchezo ulivyokwenda," Slot alisema baada ya timu yake kupoteza.

"Ilikuwa mechi yetu lakini hatukutengeneza nafasi zozote. Lazima tujiangalie, tuwe bora zaidi. Mara nyingi sana tulipoteza mpira karibu na eneo la mwisho, hatukufanya vyakutosha inabidi tubadilike na tuwe bora zaidi na mpira. Maamuzi yetu na utekelezaji wetu haukuwa mzuri . Kwa ujumla tulijilinda vizuri lakini wachezaji wawili wenye kasi walitufanya tufanye makosa."

Mbali ya kushinda na kujipatia pointi tatu, Nottingham ilikuwa imeshinda mchezo wa ligi dhidi ya Liverpool katika dimba la Anfield kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1969 ikiwa imepita miaka 55.

Bosi wa Forest Nuno Espirito Santo aliipongeza timu yake kwa kiwango ilichoonyesha na kuibuka na ushindi.

Baada ya mechi hiyo Liverpool itarejea uwanjani Jumanne kwenye Ligi ya Mabingwa, watakapokutana na na AC Milan kwenye Uwanja wa San Siro.

Mara ya mwisho Liverpool kucheza na Milan ugenini ilikuwa Desemba 2021 ambapo walishinda mabao 2-1 wakati huo wakiwa chini ya Jurgen Klopp.

Wakishamalizana na Milan watarudi England wikiendi ijayo kucheza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Bournemouth.

Chanzo: Mwanaspoti