Meneja wa Kitengo cha Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema timu hiyo imefufukia Uganda baada ya kuipiga Vipers FC bao 1-0 katika mchezo wa tatu wa Kundi C wa Kombe la mabingwa Ulaya.
Ahmed amebainisha kuwa katika mechi inayofuata ambayo ni marudiano dhidi ya Vipers, wanakwenda kuamua hatma ya timu hiyo kusonga katika hatua ya robo Fainali ya ya Mabingwa Afrika.
"Simba miaka yote kikwazo chetu imekuwa kuvuka Robo Fainali kwenda Nusu Fainali lakini sio kuishia Makundi. Hatupo tayari kuishia hatua ya makundi. Tulikwenda kuchukua alama tatu kwa Vipers lakini hatujamaliza, tunakwenda kuzichukua alama zingine hapa nyumbani. Niseme tu tuko tayari kwa mchezo" Ahmed Ally.
Ahmed ameyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari huku akisisitiza kuwa hawako tayari kuishia hatua ya makundi.
"Tulikwenda kufufukia Uganda, na kweli tumefufuka. Jumanne ni mechi ya marudio katika mechi hii tunakwenda kuamua hatma ya Simba kwenye michuano ya CAF. Tukimpiga tutafikisha alama 6 na kuanza kuchungulia robo fainali," amesema Ahmed Ally.
Katika michezo mitatu ya kundi hilo ambayo SImba imecheza imeshinda mchezo mmoja tu huku ikipoteza michezo miwili, hivyo Wekundu hao wamedhamiria kupambana na kuhakikisha wanatoboa hatua inayofuata ya robo fainali.