Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walimu shule ya Jumuiya ya Wazazi CCM Mbeya wagoma

Ivumeeeeeeeee Walimu wa Shule ya Sekondari Ivumwe jijini Mbeya wakiwa na mabango nje ya shule hiyo

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: Mwananchi

Walimu wa Shule ya Sekondari Ivumwe jijini Mbeya, wamegoma kuendelea na kazi huku wakiziba geti la kuingia shuleni humo kwa magogo wakishinikiza kulipwa fedha za mishahara na malimbikizo ya posho.

Hayo yamejiri leo Jumanne Julai 30, 2024 katika shule hiyo inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi wa CCM Mkoa wa Mbeya.

Mmoja ya walimu hao akizungumza kwa niaba ya wengine kwa sharti la kutotajwa jina lake, amesema mgomo huo ni endelevu na utafika ukomo baada ya kulipwa madai yao.

"Tunadai stahiki zetu ikiwamo mishahara na malimbikizo ya posho zetu. Tumevumilia kwa kipindi kirefu tutarejea kazini baada ya kuelezwa hatima yetu,"amesema.

Mwananchi imemtafuta mkuu wa shule hiyo, Oscar Mwaihaba kuzungumzia madai hayo, lakini amesema atafutwe baadaye kwa sasa yupo kwenye kikao.

Kufuatia sakata hilo, Jeshi la Polisi limelazimika kuingilia kati kuondoa magogo yaliyowekwa kwenye geti la shule hiyo sambamba na kufanya mazungumzo na walimu na watumishi ili kurejesha amani.

Chanzo: Mwananchi