Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara Musoma wafunga soko kisa ni hiki....

Soko Musoma Kisa (600 X 419) Wafanyabiashara Musoma wafunga soko kisa ni hiki....

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara wa Soko Kuu la mjini Musoma mkoani Mara wamegoma kufungua soko wakishinikiza kuondolewa kwa wamachinga ambao wamekuwa wakipanga bidhaa nje ya soko hilo.

Wafanyabiashara hao wamedai kuwa wateja wao wamekuwa wakiishia kununua bidhaa nje ya soko hali inayosababisha wao kushindwa kuuza bidhaa zao, hivyo kukaa muda mrefu na kuharibika.

Wamesema Wamachinga wamekuwa ni mwiba katika biashara zao, kwani wamekuwa wakiuza bidhaa zote zinazopatikana ndani ya soko hilo kwa bei ya chini.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari Wafanyabiashara hao wameitaka Serikali kuwaondoa Wamachinga katika eneo hilo ili nao wapate wateja.

Wamesema wao wanalipa kodi ya kizimba pamoja na ushuru wa soko, hivyo kukosa wateja kunasababisha washindwe kupata fedha za kulipia. 20h

Chanzo: www.tanzaniaweb.live