Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kugharamia mazishi ya aliyeuawa na polisi Simiyu

Kifo Kifo Mauiaji.png Serikali kugharamia mazishi ya aliyeuawa na polisi Simiyu

Fri, 23 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenan Kihongosi amesema Serikali itagharamia mazishi ya Kijana Meshack Daudi Paka (21) ambaye amefariki kutokana na kupigwa risasi wakati Polisi wakiwatawanya Wananchi waliofanya maandamano huko Lamadi, Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.

“Leo tumekwenda kumtembelea Mzazi wa Mtoto ambaye amefariki, tumekutana na Baba wa Mzazi, tumekutana na Familia yake tumezungumza nao na tumekubaliana kwa amani na upendo kabisa na familia imeelewa baada ya kueleweshwa kila kitu, nimetoa maagizo kwamba Serikali ibebe gharama zote za msiba ule, pili Serikali itabeba gharama zote za wale Watu ambao wamejeruhiwa”

“Na mwisho wa siku tutaliachia Jeshi la Polisi kusimamia sheria kama inavyotaka ili wale waliohusika na uhalifu, uvunjifu wa amani kwa sababu kuna vifaa vimeibwa katika Ofisi ya Uhamiaji kuna computer na vitu vingine, na wale ambao wamedhuru Watu basi tuone kwa namna gani tunaweza kuchukua hatua”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live