Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ripoti yatoa sababu barabara kupasuka Kigoma

Barabara Kupasuka Ripoti yatoa sababu barabara kupasuka Kigoma

Fri, 12 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ripoti ya uchunguzi iliyofanywa na wataalamu wa miamba kutoka Taasisi ya Geolojia na utafiti wa madini Tanzania (GST), TANROADS, na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutokana na Kipande cha barabara chenye urefu wa mita 50 kupata mipasuko mikubwa eneo la Busunzu, wilayani Kibondo, mkoani Kigoma mwezi Februari mwaka huu imebainisha kuwa mipasuko hiyo ilitokana na sababu za kijiolojia na si makosa ya mkandarasi wa mradi huo.

Ripoti hiyo imepokelewa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Innocent Bashungwa ambaye amewaagiza TANROADS kuhakikikisha wanafanya usanifu wa barabara kwenye maeneo korofi wakati wa mvua kwa kushirikiana na wataalamu wa miamba ili kubaini tabia za maeneo hayo na kuepuka changamoto zinazojitokeza.

“Nimepokea taarifa za kitaalamu na nimejionea zaidi ya mita 200 namna ambavyo majanga ya asili yaliyoathirika eneo hili, Serikali iliunda jopo la kufanya utafiti wa kina kuanzia mwezi Februari na tulichokigundua hapa sio makosa ya Mhandisi, sio upigaji kama watu wengine walivyodhani”, amesema Bashungwa.

Diwani wa Kata ya Busunzu Wilayani Kibondo, Paul Ngomagi amesema hapo awali wananchi walikuwa wanaitumia barabara hiyo katika shughuli zao za kila siku ambapo walikuwa wakitumia dakika 45 kutokea Busunzu hadi Kibondo Mjini lakini baada ya kutokea changamoto hiyo eneo Hilo wananchi wamekuwa wakisubiria hatua za Serikali zitakazochukuliwa kurekebisha eneo hilo lililoporomoka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live