Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Macha aanika uozo wa madiwani mikopo asilimia 10

Anamringi Macha Dcsd RC Anamringi Macha

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha ameanika vitendo vya uvunjifu wa sheria za mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri vinavyofanywa na baadhi ya madiwani mkoani humo, ikiwa ni pamoja na kuunda vikundi binafsi ambavyo havirejeshi fedha hizo.

Macha alibainisha hayo juzi katika kikao maalumu cha baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kahama cha kupitia na kujadili hoja mbalimbali za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2022/2023, na kupata hati safi baada ya kujibu kikamilifu hoja 25 za mwaka huo.

Alitaja moja ya kesi aliyokutana nayo kuhusu diwani (jina limehifadhiwa) aliyeunda kikundi hewa cha watu watano na kuomba mkopo wa Sh. milioni tano kwa kushirikiana na ofisa maendeleo ya jamii, baada ya kuzipata aliwapatia wajumbe wake kila mmoja Sh. 100,000 na yeye kubaki na Sh.milioni 4.1.

Alisema fedha hizo alizitumia kununua pawatila la kilimo ambalo nalo halikuweza kudumu na kuharibika na mwisho wake liliibiwa na watu wasiofahamika na hakuweza kuurejesha mkopo huo mpaka pale ofisa maendeleo alipohamishwa kituo cha kazi.

Macha alisema ofisa maendeleo mpya alianza kufuatilia kikundi hicho kutokana na kutokurudisha fedha hizo na kubaini hujuma hizo zilizofanywa na diwani.

“Tulimwita diwani tukamhoji na akakiri kuchukua fedha na sasa amekubali kuzilipa fedha zote na anaendelea na marejesho yake,"alisisitiza Macha.

Ofisa Maendeleo wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Robert Kwela alisema kwa sasa hana vikundi hewa na badala yake wale wanaoshindwa kulipa kwa muda viongozi wao wanafikishwa mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live