Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miti bilioni 1 kunusuru saruji Mlima Kilimanjaro

Mlima Kilimanjaro Intaneti.png Miti bilioni 1 kunusuru saruji Mlima Kilimanjaro

Wed, 28 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Dunstan Kitandula amesema katika kutekeleza mkakati wa muda mfupi wa kunusuru theluji inayotoweka katika Mlima Kilimanjaro, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeanzisha kampeni maalumu ya kupanda miti zaidi ya Bilioni moja katika mikoa ya Kaskazini pamoja na kupanda miti takribani Milioni nane katika Mkoa wa Kilimanjaro ili kunusuru theluji hiyo.

Naibu Waziri Kitandula ametoa kauli hiyo Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi aliyetaka kufahamu ni upi mkakati wa muda mfupi wa Serikali wa kunusuru theluji ya Mlima Kilimanjaro.

Amesema sababu ya kupungua kwa theluji katika Mlima Kilimanjaro imechangiwa na ongezeko la joto ulimwenguni lililosababishwa na mabadiliko ya tabianchi yanayotokana na shughuli za kibinadamu kama utakataji miti, kilimo na uchomaji moto katika maeneo yanayozunguka mlima, uwepo wa mvua chache na vipindi vya ukame na upepo mkavu kutoka Baharí ya Hindi.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kitandula ameweka wazi mikakati mingine ya Serikali ya kukabiliana na tatizo hilo kuwa ni Serikali kuendelea kutoa elimu ya umuhimu wa kupanda miti na uhifadhi wa mazingira kupitia vipindi vya redio na televisheni, matamasha na maadhimisho mbalimbali pamoja na kushirikiana na mashirika ya kikanda na kimataifa katika kuhimili na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo kupunguza matumizi ya gesi chafu na kurejesha ekolojia katika maeneo yanayozunguka Mlima Kilimanajro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live