Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Minara 758 kuwanufaisha waishio vijijini kwa mawasiliano

Manara Amlilia Nape Wizi Wa Bando Kwa Makampuni Ya Simu.jpeg Minara 758 kuwanufaisha waishio vijijini kwa mawasiliano

Mon, 15 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchini 8,512, 952 waishio Vijijini watanufaika na huduma ya mawasilino pindi ujenzi wa minara 758 Nchini utakapokamilika mwaka 2025 na kuwawezesha nao kupata huduma mbalimbali za mtandao.

Hayo yamesemwa leo July 15, 2024 katika kikao cha kupokea taarifa za mawasiliano kwa Mkoa wa Kigoma baada ya Waziri wa Habari na Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kuanza ziara ya siku moja Mkoani humo.

Nape ameanza ziara ya kukagua kazi za ujenzi wa minara hiyo kwa mikoa ya Kigoma, Kagera, Geita, Mwanza na Shinyanga.

Amesema kukamilika kwa minara hiyo kutatoa fursa kubwa kwa Wananchi wa Vijijini kwani nao wana haki ya msingi ya kupata mawasiliano kama Wananchi wa maeneo mengine katika uchumi wa kidigitali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live