Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama apokonywa Mtoto na Fisi

Mtoto Wa Miaka 10 Avamiwa Na Kuliwa Na Fisi Hadi Kufa Mama apokonywa Mtoto na Fisi

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto mwenye umri wa miezi nane ameuawa na Fisi baada ya Fisi huyo kumshambulia Mama yake na kumnyang’anya Mtoto huyo aliyekuwa mgongoni kwa Mama yake na kutokomea nae porini.

Fisi huyo alivamia katika vijiji viwili huku akijeruhi pia Watu wengine wanne Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara baada ya kuvamia Makazi ya Watu ambapo amejeruhi pia mifugo.

Tukio hili limetokea usiku wa kuamkia June 20,2024 ambapo juhudi za Wanakijiji zimefanikisha kumuua Fisi huyo.

Hatua hiyo imemlazimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga wakati akiwa Katika ziara yake Hospitali kuwajulia hali majeruhi wa tukio hilo huku akisema Serikali itagharamia matibabu yao pamoja na kutoa rambirambi kufuatia kifo cha Mtoto huyo.

Ametoa maelekezo kwa Watu wa TAWA kufanya ukaguzi katika kijiji hicho ili kufahamu kama kuna Wanyama wakali na kuchukua hatua huku akiwata Wananchi kutembea kwa makundimakundi katika kipindi hiki hasa kama wanakwenda maeneo yenye umbali mrefu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live