Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yazuia vijiji Ngorongoro

Ngorongoro 3.jpeg Mahakama yazuia vijiji Ngorongoro

Fri, 23 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imesimamisha utekelezaji wa amri iliyokuwa imetolewa na Serikali kupitia tangazo la Serikali namba 673 ya 2024 la kufuta vijiji, kata na vitongoji pamoja na kusitisha tangazo la kuwataka Wananchi kuhama katika Wilaya la Ngorongoro.

Uamuzi huo umetolewa jana Agosti 22, 2024 mbele ya Jaji Mwenda wa Mahakama hiyo katika kesi namba 59630 ya mwaka 2024 kufuatia maombi yaliyopelekwa Mahakamani na Mpeleka maombi lsaya Ole Posi ya kuiomba ipime na kutazama kama amri ile ilikuwa halali au la hasha au kama ilitolewa na Mtu mwenye Mamlaka ya kisheria kufanya hivyo.

Wakili wa kujitegemea Peter Njau akimuwakilisha Mteja wake Isaya Ole posi amesema Mteja wake alikuwa Mwathirika wa kuondolewa katika eneo hilo jambo ambalo aliamua kwenda Mahakamani kupinga kitendo hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live