Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lissu aibuka na wanaotimuliwa kwenye maeneo ya karibu na hifahdi

Lissu Pic Lissu aibuka na wanaotimuliwa kwenye maeneo ya karibu na hifahdi

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara Tundu Lissu ameishauri serikali kuhakikisha wanapotenga maeneo ya hifadhi washirikishe Wananchi wa maeneo husika ili kazi ya uhifadhi ifanywe na Wananchi wenyewe badala ya kupanga mipango ya uhifadhi na kutenga maeneo bila kushirikisha wahusika kama inavyofanywa sasa jambo linalopelekea uwepo wa migogoro ya mara kwa mara baina ya Wananchi na mamlaka za uhifadhi

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Chama hicho uliofanyika Mganza, Chato Mkoani Geita, Lissu aliyepo kwenye kampeni ya '+255 Oparation Katiba mpya, Okoa Bandari zetu' amewaeleza Wakazi wa eneo hilo kuwa anafahamu wana uwezo wa kutunza hifadhi ya Ziwa Viktoria kwakuwa ni Ziwa lao na wanajuwa umuhimu wa raslimali zilizopo kwenye Ziwa hilo ikiwemo uwepo wa Kisiwa cha Rubondo

"Wewe wa Ukerewe unaendaje kuwa Muhifadhi mkuu wa Ngorongoro kwenu hakuna hata Digidigi?, Kwahiyo kazi ya uhifadhi na jukumu la uhifadhi wa mazingira linatakiwa liwe wajibu na haki ya watu wanaoishi kwenye maeneo yanayotakiwa kuhifadhiwa..."

Amesema endapo wenyeji wataachiwa majukumu ya uhifadhi na kwakuwa wanafahamu kuwa hilo ni eneo lao la kupatia ridhiki hawataharibu lakini ikiwa kinyume chake wenyeji hao wanaweza kugeuka kuwa watumiaji haramu wa eneo hilo ikiwemo kutumia baruti pindi wanapopata nafasi ya kuvua Ziwani

"Kwa sababu hii mali mnaiona sio ya kwenu tena, mlinyang'anywa na mnateswa kwasababu ya hifadhi yenu mkipata nafasi ya kuweka sumu ili mvue haraka mtaweka sumu ili samaki wafe uwapate haraka, unaenda kulisha watu sumu..."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: