Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lisborn auawa kwa kuchomwa kisu na marafiki zake

Kisu.jpeg Lisborn auawa kwa kuchomwa kisu na marafiki zake

Tue, 16 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana aliyefahamika wa jina la Lisborn Adam Selemani ­(16) mkazi wa mtaa wa Nyerere Road Kata ya Kalangalala Halmashauri ya mji Geita mkoani Geita ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali na vijana wanaosadikika kuwa ni marafiki zake.

Baba mzazi wa kijana huyo Adam Selemani amesema kijana wake alichomwa na kitu kinachosadikika kuwa ni kisu wakati akiwa na marafiki zake majira ya jioni siku ya Jumapili ya Julai 7, 2024 wakiwa maeneo ya Machinjio ya zamani mtaa wa Ujamaa

Amesema kuwa kijana huyo alivyopelekwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita iliyopo Magogo alifanyiwa upasuaji mara tatu ndipo siku ya Jumapili ya Julai 14 kijana huyo alipoteza maisha.

“Kijana wangu alivyonisimulia wakati yupo hospitali alisema alivyochomwa baada ya kumpata tukio hili alitaka akimbie akajua amejeruhiwa kidogo lakini alishindwa akaanguka barabarani.

"Kuna mama mmoja ndo alimkuta akiwa analilia maumivu akamwambia bodaboda mpeleke mtoto huyu hospitali inaonekana kajeruhiwa walifikiri kachomwa na chuma kumbe ni kisu," amesema baba wa marehemu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live