Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lema akomaa na madereva bodaboda

Lema Bodabodaaa.jpeg Lema akomaa na madereva bodaboda

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema hawezi kufuta kauli yake ya kusema 'kazi ya bodaboda ni umaskini' kwani kauli yake hiyo ni sahihi.

Lema alitoa kauli hiyo hivi karibuni baada ya kurejea kutoka uhamishoni nchini Canada alikoishi kwa zaidi ya miaka miwili akidai kuwa kazi ya kuendesha pikipiki imesababisha uyatima, umasikini, vifo na ukilema kwa wanaotoa huduma hiyo.

Aidha, Lema alidai kuwa Serikali inapaswa kuweka mifumo madhubuti ya ajira badala ya vijana kutegemea bodaboda.

Hata hivyo chama cha waendesha bodaboda Arusha walijitokeza na kumtaka mwanasiasa huyo kuomba radhi.

"Nikimuona mtoto wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa au Mtoto wa Rais Mwinyi anaendesha bodaboda na kudai ni kazi ya heri nitaomba radhi.

"Bodaboda ni kazi ya mateso,imeumiza watu na kujeruhi watu wengi. Acheni kudanganywa na Serikali iliyo kosa mbinu za kuokoa maisha yenu. Umasikini sio sifa," amesema Lema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: