Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Latra kuanzisha utartibu mpya wa usafiri Dar

Daladala Nguvu Nguvu.png Latra kuanzisha utartibu mpya wa usafiri Dar

Wed, 14 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra), inatarajia kuanzisha huduma ya ‘Ride Sharing’ kabla ya kuisha mwaka huu wa fedha 2024/25.

Watu tisa hadi 14 wataweza kupanda gari moja kwa kuomba kupitia mitandao ya simu hata kama wapo vituo tofauti.

Akizungumza Jumanne, Agosti 13, 2024 Mkurugenzi wa Udhibiti Usafiri wa Barabara wa Latra, Johansen Kahatano amesema wameamua kuja na huduma ili kuendelea kuwarahisishia wakazi wa Jiji la Dar es Salaam usafiri lakini pia wameona kuna uhitaji mkubwa wa huduma hiyo.

Kahatano amesema tayari baadhi ya mitandao ya simu imeonyesha utayari wake katika utoaji huduma hizo.

“Tunafanya yote haya ili kuwarahisishia wananchi usafiri na kuwa na chaguo, kwa wale ambao wanataka kupanda usafiri wa hadhi watapanda na wale wenzangu na mimi basi watapanda ule wa daladala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live