Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiteto yapewa mamilioni kwa miradi

Kiteto Qwe Kiteto yapewa mamilioni kwa miradi

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali kuu imetoa Sh. milioni 949.2 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani hapa Mkoa wa Manyara.

Mbunge wa Kiteto, Edward Ole Lekaita Kisau, aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na wananchi wa eneo hilo.

“Ndugu wananchi wenzangu wa Jimbo la Kiteto, nachukua fursa hii, kuwafahamisha tumepokea Sh. 949,200,000 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Nimezungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa na amethibitisha pesa zimetumwa na Mkurugenzi wetu wa Halmashauti ya Wilaya ya Kiteto, Hawa Hassan Abdul, amenithibitishia kupokea fedha hizo na zitatumwa kwenye maeneo husika bila kuchelewa,” alisema Ole Lekaita.

Alisema fedha hizo zitatumika kwa ujenzi wa shule ya msingi mpya ya Olmugi iliyopo Kata Namelock na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya vyoo shule za msingi Orgira Kata ya Sunya.

Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya vyoo shule ya msingi Nalangitomon iliyopo Kata ya Partimbo.

Vyumba vitatu vya madarasa, matundu sita ya vyoo na madarasa na vyoo ya mfano ya awali shule ya msingi Kurash,Kata ya Lengatei.

Vilevile zitatumika kwa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya vyoo shule ya msingi Enguserosidan ya Kata ya Laiseri.

“Tutajenga vyumba vitatu vya madarasa na matundu sita ya vyoo shule za msingi Orkitikiti (Engangongare), Kata ya Lengatei,” alisema.

Mbunge huyo, alisema fedha hizo, zitatumika kujenga nyumba ya walimu katika shule ya sekondari ya Ndirigish kwenye Kata ya Ndirigish.

“Kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Kiteto, tunamshukuru sana Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote serikalini kwa kutupatia kiasi hiki cha fedha kwa kuwa zitakwenda kuchochea shughuli za maendeleo kwa wananchi.

“Pia tunamshukuru rais wetu, kwa kuendelea kuboresha maisha yetu, wana Kiteto kwa kuendelea kutuletea miradi mikubwa ya maendeleo na kushughulikia changamoto za wananchi katika wilaya yetu,” alisema Ole Lekaita.

Akizungumzia kuhusu ahadi za Chama Cha Mapinduzi (CCM), alisema zinaendelea kutekelezwa kwa kushirikiana wananchi wa Kiteto na wana sababu ya kutoa shukrani kwa Rais Samia.

Alitoa wito kwa watumishi na wananchi kuhakikisha miradi hiyo inalindwa na kusimamiwa vizuri na kwa ufanisi ili kulenda maendeleo na watu wapate huduma hizo kwa wakati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live