Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Pangani avalia njuga vitendo vya ubakaji, ulawiti

Mussa Kilakala DC Pangani avalia njuga vitendo vya ubakaji, ulawiti

Tue, 25 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa wilaya ya Pangani Mussa Kilakala ameanza kuvalia njuga vitendo vya ubakaji na ulawiti huku akiliagiza Jeshi la Polisi wilayani humo kumfuatilia na kumkamata mtu mmoja kwenye kijiji cha Bushiri ambaye ameripotiwa kwa tuhuma za kuwashawishi watoto wa kiume ili afanye nao vitendo hivyo.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa wilaya amepiga marufuku uuzwaji wa pombe majumbani ambao umebainika kuwa chanzo cha ukatili wa kijinsia kwa familia hususani wakati ambao watu wanaanza kulewa.

Kilakala ametoa maagizo hayo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM wilaya ya Pangani huku akiitaka jamii kuungana kuhakikisha wanafanikiwa kwenye vita dhidi ya ukatili huo kwa watoto.

"Ndugu Mwenyekiti nilikwenda kwenye shule moja ( jina lake limehifadhiwa) hapa Bushiri mtoto mmoja jasiri, tungekuwa na watoto majasiri kama yule hili tatizo lingekwisha kabisa kwa muda mfupi, yule mtoto alizungumza kwa uchungu nadhani alikuwa form 3 au form 4 ameonyesha maigizo akaimba baadae akachukua maiki na kuzungumza kunambia mkuu wa wilaya mimi binafsi nimefanyiwa ukatili wa kijinsia kuna mzee ananitaka mimi kimapenzi hali yakuwa anajua mimi ni mtoto wa kiume," amesema DC Kilakala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live