Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Magoti awasha moto "Mnalaza watoto 96 msikitini? FUnga kituo"

DC Magoti Fdsg DC Petro Magoti.

Fri, 12 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama wametoa saa 24 kwa kituo kinachotoa mafundisho ya Dini ya Kiislamu katika Msikiti wa Masjid Salaf uliopo Kiluvya Madukani, kufunga kituo hicho na kuwarejesha Watoto kwa Wazazi wao hadi watakapojenga mabweni na kupewa kibali maalum cha kuendesha mafunzo hayo.

Hii ni baada ya kubaini Watoto zaidi ya 90 wanalazwa katika eneo dogo Msikitini na wengine nje ya Msikiti huku mazingira wanayopikia chakula na yanayowazunguka yakiwa hatarishi na machafu.

Kiongozi wa kituo hicho, Sheikh Abdul Hamid amesema kituo hicho kimeanza kutoa mafunzo tangu Mwezi May 2022 na wanapata Watoto kutoka Mikoa mbalimbali ambapo baada ya Timu ya DC Magoti kuwahesabu Watoto waliokuwa Msikitini kwa wakati huo wamebaini Watoto 25 wanatoka Mtwara, Singida Watoto 15 , Morogoro tisa, Pwani wawili, Tunduru mmoja, Tabora wawili, Lindi wawili, Tanga watatu , Iringa watano , Kigoma wawili, Dar es salaam mmoja na Mtoto mmoja Raia wa kigeni kutoka Kenya.

DC Magoti baada ya kukagua eneo hilo amesema “Sasa unabananisha Watoto kama nyanya, tumekuja Kiluvya hapa kuna Watoto 96, lengo la Sheikh ni nzuri, Dini yetu ni nzuri lakini matumizi ya hawa Watoto sio sahihi.

Hapa ni hatari anaweza kutokea nyoka, Mtoto akaugua Malaria, akaugua Kipindupindu, Watoto 96 wanapangwa kama nyanya kama tofali za block, halafu Mzazi unamleta Mtoto, hujui Mtoto anaishi wapi?, analalaje?, anakulaje? “, kuna Watu wanatafuta uzazi wanazunguka Dunia nzima kutafuta Watoto, magodoro yanaisha Mtu anatafuta Watoto, wewe Mtoto wako unamtelekeza anakuja kuishi haya maisha”

Katika hatua nyingine baada ya kutoka Masjid Aslaf, DC na Timu yake wamefika Msikiti mwingine unaoitwa Masij Abdulaziz Ashlak ambako nako wamebaini Watoto wakiwa wanalala kwenye mazingira yasiyo rafiki na salama.. kutazama video yote kwa urefu ingia Youtube ya MillardAyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live