Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Magoti apiga marufuku ngoma, muziki kwa wanafunzi

DC Magoti Fdsg DC Magoti apiga marufuku ngoma, muziki kwa wanafunzi

Tue, 25 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti amepiga marufuku Watu kuandaa shughuli za ngoma kama vile mdundiko, unyago na sherehe za muziki na kuruhusu Wanafunzi kujumuika na kuserebuka kwenye shughuli hizo ambapo amemuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya hiyo kwamba vitendo hivyo vikibainika akamate kuanzia Mpiga ngoma, Wazazi wa Mtoto, aliyepewa tenda ya muziki hadi gari lililobeba muziki huo.

Akiongea Wilayani Kisarawe wakati akikabidhiwa ofisi rasmi na DC Fatma Nyangasa, Magoti amewataka pia Walimu wanaoanzisha mahusiano ya kimapenzi na Wanafunzi wao kujiandaa kwani akiwabaini atawashughulikia “Mh. OCD kwa wale Viongozi wako ngoma ikikutwa anachezwa Mwanafunzi, kamata anayepiga ngoma, kamata Mama, kamata aliyepeleka muziki, gari lililopeleka muziki peleka kituoni”

“Kama Mtu anapewa tenda ya kuchezesha ngoma kwa Wanafunzi waambie wasiende, tutakamata gari, tunafika Polisi pale usiku tunatoboa matairi upepo hamna muziki utaletwa hapa Halmashauri, sasa utatuambia DC kapokonya vitu si kuna sheria ya kuhatarisha, sikiliza ile clip ya Mh. Mkuchika ameelezea vizuri Mtu anayehatarisha amani kwasababu wewe unafanya Watu wawe Wajinga wasisome unahatarisha amani, tunadili na wewe vizuri sana”

“Nimesikia kuna Walimu wanapenda Wanafunzi sitaki kuwahukumu sijafika naendelea kupokea data zangu kama wewe unatafuna Watoto wetu ambao yaani wewe, Mh. Rais analeta pesa yule Mtoto anakula anavaa anapendeza, yaani Mh. Rais anatoa matumizi wewe unakula!, serious?, halafu Mh. Rais anakulipa mshahara, umepewa nyumba ya Serikali unaishi, umeme upo”

“Mtu wa Maendeleo ya Jamii upo wapi?, malezi hapa ni zero, una Watoto? Mwanao yupo darasa la ngapi?, chekechea?, sasa fikiria Mwanao yupo darasa la tatu akapigwa mimba utajisikiaje?, si vibaya? ndio rahisi anavyojisikia vibaya hivyo kusikia Watoto wana mimba, kwahiyo andaa utaratibu wa semina na mikutano ya darasa la maadili kuanzia July mwaka huu kila Shule tuwe na mambo ya maadili, Mtu yoyote anayetaka kuweka nguvu kuhusu unyanyasaji wa kijinsia twende nae, ukiona Mtu ananyemelea kabinti kashule njoo niambie huyu alikuwa na Mtoto nimemuona anamshika chuchu tutamshughulikia vibaya mno”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live