Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodaboda wamkaba Lema

Bodaboda Tangad Bodaboda wamkaba Lema

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Madereva na Wamiliki wa Pikipiki Tanzania (CHAMOPITA), Mkoa wa Tanga, kimemtaka Mwenyekiti wa CHADEMA, Kanda ya Kaskazini Godbless Lema kuwaomba radhi ndani ya siku saba kufuatia kauli yake kuwa kazi ya bodaboda ni biashara iliyolaaniwa na pia haijarasimishwa.

Lema alitoa kauli hiyo hivi karibuni mkoani Arusha, wakati aliporejea nchini kutoka Canada na kupokelewa na wafuasi wa chama chake.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga, Mwenyekiti wa CHAMOPITA, Michael Renatus amemtaka kiuongozi huyo wa kisiasa arudi kwenye vyombo vya habari, ili kukanusha kashfa hiyo kwa kundi la bodaboda nchini.

“Kitu ambacho kimetufanya tufike hapa ni pale alipotoa kauli tata sasa sisi kama chama tunamtaka arudi kwenye vyombo vya habari akakanushe kauli aliyoisema au atuombe radhi ndani ya siku saba, endapo hatafanya hivyo chama cha bodaboda kitafanya maandamano nchi nzima kupinga kauli za mwanasiasa huyo,”amesema Renatus.

“Kama sio kazi rasmi mbona bodaboda ndio ambao walimpokea kutoka uwanja wa ndege? Tumeumizwa na kauli zake ambazo zina lengo la kuleta uchonganishi kati yetu na serikali,” amesema.

Kwa upande wake muasisi wa bodaboda Wilaya ya Tanga mjini, Bakari Masakuzi amelaani kauli hiyo kuwa ni ya ubaguzi, wakati kazi yao imekuwa inawasaidia kwenye maisha ya kila siku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: