Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodaboda alietoweka siku tano, Mwili wake waokotwa Shambani

Boda Boda Moshiiiii Bodaboda alietoweka siku tano, Mwili wake waokotwa Shambani

Sat, 20 Jul 2024 Chanzo: Mwananchi

Dereva wa bodabodo, Jackson Ngowi (24), mkazi wa Kijiji cha Maharo, Kata ya Makiidi, Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, aliyetoweka kwa siku tano, mwili wake umekutwa ukiwa umetelekezwa kwenye moja ya shamba lililopo katika Kijiji cha Ngambeni ukiwa umeharibika.

Kijana huyo anadaiwa kutoweka Julai 14, 2024 baada ya kukodiwa na mtu asiyefahamika, huku wenzake kijiweni kwake anakofanyia kazi wakidhani ni abiria wa kawaida.

Baada ya kuondoka na mteja huyo hakuonekana tena kijiweni hapo wala nyumbani kwao, mpaka mwili wake ulipokutwa juzi jioni ukiwa umetelekezwa kwenye shamba hilo.

Taarifa zinadaiwa baada ya kutoonekana nyumbani kwao, jitihada za kumtafuta zilifanyika sambamba na kutoa taarifa Kituo cha Polisi Mkuu.

Hata hivyo, simu zake na pikipiki yake hazijulikani zilipo.

Akizungumza na Mwananchi jana Ijumaa Julai 19, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema baada ya kijana huyo kutoweka nyumbani kwao, familia ilitoa taarifa polisi ambalo lilimsaka kabla mwili wake kuokotwa jana jioni.

Kamanda Maigwa amesema tayari wamefungua jalada la uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Chanzo: Mwananchi