Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto Kabwe: Kauli ya Rais Samia inavunja Katiba ya Nchi

Zitto Kabweee Bact Act.png Kiongozi wa Chama Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe.

Sun, 11 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa Chama Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ametoa wito kwa Serikali kuwalipa fidia wananchi wanaotoa ardhi, mashamba au makazi yao kupisha miradi ya Maendeleo. Amesema fidia ni suala la kikatiba viongozi wa Serikali wasivunje Katiba ya nchi kwa kukataa kulipa fidia.

"Unapopitisha mradi wa reli halafu usiwalipe watu fidia kwa kisingizio cha mradi wa maendeleo unavunja katiba; na kuvunja katiba ni jambo ambalo halipaswi kuvumiliwa 'uncompromised'." Amesisitiza Zitto.

Kiongozi huyo ameyasema hayo akiwa katika Jimbo la Bukene Mkoani Tabora akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.  

Ameongeza kuwa "Kwa hiyo nataka kutoa wito kwa Serikali watu ambao ardhi zao, mashamba yao yamepitiwa na mradi wowote iwe SGR (Reli ya kisasa), barabara, iwe ni Shule, hospitali n.k. wafanyiwe tathmini inavyostahiki na walipwe fidia inavyostahiki."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live